KIGENI KWAKO KISIKUPE ASILIMIA ZOTE KAMA HUJAKIJUA.


Unaweza ukamfurahia mtu ukiwa humjui, ukaona anakufaa kuwa rafiki yako wa karibu katika kukushauri mambo mbalimbali ya maisha kwa jinsi ulivyomwona kwa nje.

Siku ukijenga ukaribu naye wa mawasiliano/mazungumzo, unaweza usione ule uzuri uliokuwa unauona awali vile vile unaweza ukafurahia umhimu wa huyo mtu na kuona anakufaa zaidi ya vile ambavyo hukuzania.

Asilimia kubwa ya watu ni wazuri mdomoni, na wazuri kwenye macho yaani ukimwona unampa maksi zote kuwa ni mtu sahihi kwako, ila baada ya kujenga ukaribu naye unaweza ukabaki mdomo wazi na usimkubali tena.

Tunajifunza nini katika hili, uhalisia wa mtu haupo vile unavyoweza kumtafasiri kwa macho au kwa maneno yake ya siku moja.

Unahitaji kumpa muda na kumwangalia nyendo zake, je zinalingana na yale unayoyaona ama ni zile za kufanya usafi kwa kuweka mazingira sawa siku mtu amesikia atakuwa na ugeni mkubwa.

Kuna maeneo hutakiwi kumwamini mtu haraka, na kuna maeneo unahitaji kujipa muda kumwelewa mtu. Ukisema ya nini nijisumbue, usije ukatumia kauli ningejua.

Ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku, ukiona macho yamevutiwa sana na kitu fulani usikipe asilimia zote, hebu tulia kwanza na uchunguze yaliyomo yamo? unapoendelea kuhoji kuna mengi utayagundua, maana tabia mtu huwa haijifichi hasa ukiwa makini.

Maigizo ni mengi sana kuliko uhalisia wa maisha, unaweza ukachanganywa na maigizo ukaona ndio maisha halisi ukajikuta umepotezwa.

Usiogope kuhoji na kufakari, tena hii ni tabia ya KiMungu kabisa ambayo ameturuhusu tuzipime kila roho, je ni za kweli ama za uongo.

Epuka kuingizwa matatani kwa  kumjua mtu kiundani na kufuatilia kile unachokiona kwa macho ndicho halisi ama ni danganya toto unase mtegoni.

Shika kwamba, hupaswi kuwa na hofu wala kuogopa ila unapaswa kuhoji kwa kila unachokiona kinakuvutia machoni/masikioni mwako.

Nakutakia wakati mwema.

            Samson Ernest.
  whatsApp +255759808081.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment