Usipoipa akili yako kazi ya kufanya yenyewe itakupa kazi ya kufanya.

Habari za leo mpenzi msomaji wa makala hii, matumaini yangu unaendelea vizuri kutimiza malengo yako uliyojiwekea mwaka huu 2015, kama bado hujafikia kile kiwango ulichotarajia usife moyo endelea kukazana na kuweka mipango na juhudi zako vizuri ili upate kufika pale ulipopanga kufika.

Mara nyingi kwa mazingira yetu tunayoishi kila siku, yamejaa mambo mengi sana hata mtoto anayezaliwa leo baada ya miezi kadhaa ijayo unaweza kuta anaongea vitu vya ajabu ambavyo usingeweza fikiri kama mtoto mdogo anaweza kuongea vitu vikubwa namna hiyo, hii inatokana na msongamano wa vitu vingi hapa chini ya jua vinavyoendelea.

Unapoona mtu anakuwa na mawazo mema pale anapochangia kitu ama anapozungumza kitu jua ubongo wake umelishwa vitu vya msingi na sahihi, akili yake imepewa kazi ya kumeza vitu vinavyofaa tu asilimia kubwa, mara nyingi hii haitokei tu kwa mtu pasipo kujua anatakiwa afanye nini na asifanye nini. Kama kila kitu utakubali kukifanya ujue haupo sahihi kabisa vivyo hivyo kama utaacha kuingiza chochote kizuri kwenye ufahamu wako, jua hata yale mazuri uliyoingiza mwanzo yanafunikwa na mawazo hasi yasiyo na faida kwako zaidi ya kukuangamiza.

Dunia ya leo imejaa takataka nyingi sana za kuharibu akili za watu njema kuwa mbaya, hebu chukulia upo ofisini wafanyakazi wenzako mazungumzo mengi ni kuongolea maisha ya wengine vibaya mara fulani kafanya hivi mara jana alifanya vile mara msanii fulani alifanya hivi, ukiingia kwenye mitandao unakutana na picha za ovyoovyo mwingine kapost amejiachia ovyoovyo, kama ni mdada maziwa yote ameachia nje, mwingine amejibinua ovyo, mwingine ameachia mipaja yote nje na kama ni mwanaume yeye kazi yake ni kupost vitu vya ajabuajabu amejipa majina ya ovyo sijui timu gani.

Sasa hapa usipokuwa makini na maisha yako na usipokuwa na uchaguzi sahihi wa kuchagua marafiki wa kuwa nao utajikuta ni mtu usiye na mwelekeo mzuri wa maisha yako binafsi, ili akili yako iwe na vitu sahihi na kuipa kazi ya kubeba vitu sahihi ni lazima UJITAMBUE, ni lazima ujue unatakiwa kuwa na MARAFIKI wa aina gani, ni lazima ujue VITU vya kufanya na kuepuka kufanya, ni lazima uwe mtu wa kujisomea sana vitabu, kusikiliza cd/dvd  kwa wale waliofanikiwa na kuvuka maeneo mbalimbali katika maisha yao maana pasipo kuonana nao walifanyaje wakafika hapo walipo unaweza kuonana nao kwa njia ya kujisomea nakala zao za vitabu/blogs.

Pia kwenye mitandao ya kijamii unatakiwa uwe na marafiki unaowahitaji sio kila mtu anaweza kuwa rafiki yako, sio kila rafiki anaweza kuwa rafiki, usiniambie watu wote ni marafiki zako hapo utakuwa unaidanganya akili yako labda wawe tu marafiki majina lakini rafiki unayemhitaji ni yule ambaye anaweza akakushauri jambo, yule anayeweza kukuonya pale unapokosea, yule ambaye yupo tayari kukuambia ukweli pasipo kukuficha, yule ambaye anaweza kukufundisha jambo na wewe ukamfundisha na mkaelewana... usisahau pamoja na kuwa na marafiki zako sahihi hii isiwe tiketi ya wewe kuitikia kila kitu NDIO, hapana lazima uwe mchambuzi wa vitu unavyoambiwa na unavyoshauriwa waswahili wanasema akili ya kuambiwa changanya na yako.

Ilishe akili yako maarifa sahihi ili kuisaidia kusafisha yale mawazo yasiyofaa katika maisha yako, usikubali kuridhika na ya jana ichukulie jana kama tiketi na ichukulie leo kama safari.
Nikutakie siku njema, siku yenye utofauti kabisa wa maisha yako kiroho na kimwili.

Nikutakie wakati mwema, endelea kutembelea mtandao huu MTAZAMO WA MAISHA.
Samson Ernest; 0759808081.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment