NJIA ZAKO NJEMA ZITAKUPANISHA NA MAADUI ZAKO.

Yapo mambo hatuwezi kuyakwepa, inatokea tu mtu anakujengea hila moyoni mwake pasipo wewe kujua kwanini ametenda hivyo.

Huwezi kujua ameambiwa nini juu yako akaona wewe ni mtu mbaya kwake.

Wakati mwingine maneno mabaya yanaweza kusambazwa pasipo ushahidi wowote, yakakujengea chuki mbaya kwenye mioyo ya watu.

Ikiwa wewe huna uhakika wa jambo, unajitoa kuzungumzia maisha ya mtu fulani vibaya pasipo kujua lolote. Unafikiri watu wengine watashindwa kusema juu yako.

Hawatashindwa kabisa, maana wengi wetu huwa tunapenda kuangalia upande mmoja kuliko pande zote, na kulibeba jambo hata kama hatuna uhakika nalo.

Mtu anakuja kukupa ubaya wa mtu fulani aliomtendea, ila hawezi kuusema ukweli kwanini atendewe hivyo. Inaweza kuwa ametendewa baya kweli lakini ubaya ule anaukolezea chumvi sana.

Lakini ipo njia ya kuweza kukufanya watu wale warudi wakuone wewe ni mwema kwao, hutaenda kuwagawia pesa ndio wakuone mzuri. Bali unapof anya wema machoni pa Bwana wako ndipo na yeye anazidi kukusafisha kwa wabaya wako.

Wema wako mbele za Mungu, na njia zako safi mbele zake, zitafunua matendo yako mema na kukupanisha na maadui zako waliopanga mabaya juu yako.

Najua umewahi kukutana na hili, uliambiwa mtu fulani ni mbaya sana hafai hata kukaa naye meza moja. Baadaye ukashangaa mbona niliyokuwa nasikia si kweli.

Mtu mwingine anakwambia, niliambiwa una roho mbaya sana na watu mbona matendo yako yanakataa kabisa... Hakika nimeona wewe ni mtu mwema.

Huhitaji kutafuta matangazo kwenye vyombo vya habari kuwaambia watu wewe ni mwema, huhitahitaji kuingia kila nyumba ya jirani yako kumweleza anachokupakazia sio sahihi.

Unahitaji kutengeneza mahusiano yako na Mungu wako, uhusiano wako na Mungu unaosha mambo mabaya na kukupatanisha na wengine.

Hata kama lipo jambo uliwahi kuwakosea watu pasipo kujua wewe, njia zako zinaibua yaliyo safi kwako.

Weka juhudi kutengeneza uhusiano wako na Mungu, ili wale wakusingizio mabaya juu yako wapate kuona matendo mema kila wakutazamapo.

Matendo yako yatafuta alama mbaya ndani ya mioyo ya watu, mwanzo watasema anajifanya mtu wa Mungu, baadaye watasema tumejua wewe ni mwema.

Mwanadamu huwezi kumfurahisha/kumridhisha kila eneo, ila Mungu unaweza maana yeye umkoseapo hutoa nafasi ya kutubu.

Nakutakia wakati mwema.
www.mtazamowamaisha.blogspot.com
Samson Ernest.
+255759808081.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment