SABABU INAYOPELEKEA MWANAUME APOTEZE NGUVU YA KUWA KICHWA CHA FAMILIA HII HAPA.

Habari za leo rafiki, ni siku nyingine tena tumeiona. Vipi wewe unayo furaha ya kupata fursa ya kuiona leo au unaifikiria jana ya maumivu/mateso.
Furahia siku yako, ili ufanye vitu kwa ubora wa juu zaidi, furaha ni dawa ya uchangamfu wa moyo wako, na tiba kwa fikra zako.

Karibu tujifunze umhimu wa mwanaume katika familia, nimelazimika kuaandika haya kutokana na tabia inayoendelea kwa wanaume walio wengi katika jamii zetu. Sio kusudi langu kutoa lawama kwa upande huu, nia yangu ni kukumbushana wajibu wetu tunaopaswa kufanya kama wanaume.

Kumeibuka katabia kachafu hasahasa kwa vijana wa kiume, kutunzwa na mabinti katika vyumba vyao vya kupanga/kujenga. Yaani mwanaume anatoka kwake anapoishi anaenda kuishi kwa mwanamke.
Hili unaweza kuona ni jambo la kawaida sana, ila ni jambo lenye maana kubwa sana katika kuondoa ule umamlaka wa mwanaume katika nyumba.
Huwezi kukaa kwa mwanamke, kwenye chumba chake au nyumba yake ukamwamrisha kila kitu unavyotaka wewe. Huna ile nguvu/uwezo wa kumuuliza ulikuwa wapi mbona umechelewa kurudi nyumbani kiasi hichi. Hata kama utajitutumua kuuliza ulikuwa wapi, bado ndani mwako utakuwa huna ujasiri wa moja kwa moja.

Hili la mwanaume kuhamia kwa mwanamke, mara nyingi huwa kwa mahusiano yasiyo sahihi. Yaani ni mahusiano yasiyo na kibali mbele za Mungu, inaweza kuwa mwanaume ameacha mke wake ndani ameenda nje ya ndoa ama hajaoa ila anatunzwa kwa mwanamke.
Elewa kwamba, ukiwa umekubali kukaa kwa mwanamke, uwe una pesa nyingi sana, uwe na elimu kubwa sana, uwe mjanja sana wa maneno... wewe bado utaitwa mtu aliye chini ya mamlaka ya mwanamke. Haijalishi chakula unachokila umetoa pesa wewe, wala haijalishi unatoa kodi ya nyumba wewe.
Ikiwa umekubali kubeba nguo zako, na kuacha kwako, ukamua kuhamia kwa mwanamke. Ni kipimo cha akili yako imekubali kumilikiwa na huyo mwanamke, kwa sababu Biblia yangu inaniambia mwanaume ni kichwa cha familia.

Kuitwa wewe ni kichwa, maana yake wewe ni dira ya familia, na siku zote kichwa lazima kiwe na maamzi ya kuilazimisha miguu kwenda sehemu inayotaka, kuiamuru mikono ifanye kile kilicho ndani ya taarifa ya kichwa. Ndio maana tunaona walemavu wa macho wanafanya shughuli zao kama wenye macho, ndio maana tunaona watu wasio kuwa na miguu wala mikono wanaishi vizuri tu.
Hii ni kwa sababu kichwa ni kizima, vinginevyo kingekuwa kibovu na ramani nzima ya maisha ingeharibika.

Kuna msemo mmoja unasema, kosea yote, vurungwa siku nzima, umizwa sana, ingia hasara. Ila kichwa ukumbuke kunirudisha nyumbani, hii ni kumbukumbu ya ajabu sana, na sijui kama umewahi kuifikiria hii. Kama utasahau kurudi nyumbani ukajikuta unalala sehemu isiyo kwako pasipo sababu ya msingi. Jua kuna shinda kubwa kwenye ubongo wako.

Umewahi kujiuliza kwanini mtu anaporukwa akili yaani kuwa kichaa. Kinachomfanya akibie nyumbani ni kitu gani? kwanini watu wahangaike kumfunga kamba angalau atulie. Jibu ni kwamba KICHWA chake hakina maamzi tena ya kumwendesha salama, mamlaka haina nguvu tena ya kuamrisha vingine.

Pia kuna msemo mmoja unasema, mwanaume utaendeshaje/utaamrishaje wanaume wenzako wakati wewe umeshindwa kujiendesha. Mwanamke anakuendesha, ujasiri wa kutoa sauti kama baba mwenye nyumba ni mdogo mno. Hata kama utajitutumua mbele za watu kukoroma, ukweli utabaki kuwa wewe upo chini ya mamlaka ya mwanamke.

Jiulize kwanini boss wako kazini ana mamlaka ya kukufukuza kazi, ila sio mtu mwenye maamzi ya mwisho yaani na yeye anasubiria kauli ya mwisho kwa mkuu wake atasemaje kuhusu wewe. Ndio maana siku zote, ukiwa upo karibu sana na mkuu yaani mmiliki wa kampuni/idara hiyo ni ngumu sana wewe kuguswa na mamlaka hizi za chini. Lazima watakuwa wanakuogopa badala ya wewe uwaogope.

Ndio maana ukikutana na wale wanawake wenye tabia chafu(malaya) wa kutembea na maboss kazini, huwa wana dharau fulani mbaya sana kwa wafanyakazi wengine. Ukiangalia kwa undani, unakuta wameishikilia ile mamlaka iliyokuweka wewe hapo, inayokufanya ikulipe. Imeshikiliwa kwa ngono na huyo mwanamke anayewadharau, hata kama mtamletea maneno ya kumchafua, mtayasema pembeni ila sio kwa boss wenu. Labda itokee hamjui, na kama hamjui utashangaa unahamishwa hiyo sehemu, ama unashangaa boss hakupendi, visa kila siku. Kisa nini ,umegusa mamlaka ya mkuu wako anayekupa kula.

Nikushauri kwamba usijipe moyo kwamba wewe ni kidume, wewe sio kichwa tena katika kutoa sauti ya mwenye mamlaka, bali upo chini ya mamlaka. Umewahi kujiuliza kwanini mwanaumke ana nguvu/ujasiri wa kutupa nguo zako nje pale anapokuchoka, na umewahi kujiuliza mwanaume huwa anapata wapi ujasiri wa kumtupia mke wake begi lake nje. Na hapo mwanamke anakuwa hana jeuri ya kumjibu mume wake kama anavyotaka yeye zaidi atakuwa mnyonge na mwenye kulia tu.
Na mwanaume kwanini anakuwa hana sauti ya kukemea hicho kitendo cha mke wake kumkemea na kumwambia ondoka kwangu kwa kutupa nguo zake nje.

Naona hujanielewa, wewe mwanaume uliyekaribishwa na mwanamke kwenye nyumba yake aliye jenga yeye kwa jasho lake, hata kama ni mke wako wa ndoa. Jaribu kumfukuza kwa kumwambia nenda kwenu kapumzike huko sikutaki hapa kwangu... jaribu uone, fanya hivyo sasa hivi hata kwa utani baada ya kumaliza kusoma ujumbe huu.
Sikufundishi ujinga ila najaribu kukueleza vitu vinavyowezekana kwa vitendo, maana nikikupa hadithi nyingi sana unaweza Ukaona ni uzushi tu wa mwandishi.

Nguvu yeyote unayoiona kwa mtu, ujasiri wowote unaouona kwa mtu. Huanzia ndani ya moyo wa mtu, kusema kitu pasipo kupepesa macho huanza ndani ya nafsi/moyo wa mtu. Kitu kama sio cha kwako, hata kama watu watakusifia, hata kama watu wataona ni cha kwako bado wewe ndani yako utakuwa una hukumiwa kwa kupewa sifa zisizo za kwako. Yaani nimeandika hii makala alafu wewe ukafanya ya kwako, kwa kufuta baadhi ya vitu vinavyonitambulisha mimi kama mwandishi. Hutakuwa na uwezo wa kujitetea mbele za watu, ikiwa atatokea aliyeandika.

Ukiwa unasoma ujumbe huu alafu upo miliki ya mwanamke, nakuomba ufanye maamzi ya busara. Tukiacha unafanya dhambi, naomba utambue thamani yako, ni aibu kubwa sana mwanume mzima na ndefu zako, mtu unayeonekana mkubwa mbele za jamii kuja kutupiwa nguo zako nje.
Kama wewe ni mwanaume umeoa, na upo nyumba aliyejenga mke wako. Hujachangia chochote, jitahidi ujenge ya kwako alafu hiyo ifanyeni ya kupangisha.

Ukiona ninachokisema hapa ni upuuzi, achana nacho, ila utakumbuka siku yakikutokea. Na yasipokutokea shukuru Mungu wako... wanasema bora ujiandae ukakikosa kuliko kutojiandaa ukakikuta, yaani afadhali ukaamini Mungu yupo ukaishi kama anavyoelekeza kupitia neno lake, kuliko kutoamini chochote ukaenda kumkuta yupo.

Rafiki yako Samson Ernest.
Waweza wasiliana nami kwa namba 0759 80 80 81/0715 59 15 59, email; samsonaron0@gmail.com

Nikushukuru kwa kutenga muda wako kusoma makala hii.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni: