Upweke ni tatizo linalowatesa wengi, ni tatizo ambalo limekuwa kama ugonjwa fulani hivi kwa watu wanaokabiliwa na hili tatizo.
Kuna upweke wa aina nyingi, ila upweke ambao umetawala vijana na wazee ni upweke wa kukosa mahusiano ya mke na mume. Kijana anapofika hatua ya kutaka kuishi na mwenzi wake akawa anapata shida kumpata, hili swala la upweke hutawala sana ndani yake.
Kwa wanandoa pia lipo vile vile, pale mke anapomhitaji mume wake kwa ukaribu sana ila inatokea mume hajali wala hana muda huo wa kuwa karibu na mke wake. Vivyo hivyo kwa mume anapomhitaji mke wake kwa ukaribu, mke anakuwa hana uzito huo labda kwa kutotimiziwa haja zake fulani.
Unaweza ukamhisi mtu anaumwa ugonjwa wa kwenda kutibiwa hospital ila sio kweli kila unayemwona ana tatizo hilo, unaweza kumwona mdada/mmama mkubwa kabisa lakini vitu anavyovifanya haviendani kabisa na umri wake, shida nini? upweke.
Upweke humfanya mtu ajihisi kuna mtu amebeba uhuru wake, hujihisi kuna kitu kimekosekana ndani ya maisha yake. Mtu anaweza akawa na pesa za kumfanya aishi vizuri pasipo tatizo lolote, kila hitaji la kununua analolihitaji analipata kwa wakati. Ila hili tatizo la upweke hawezi kuliondoshwa na pesa hizo.
Usifikiri kila unayemwona hana furaha/uchangamfu ukafikiri ameumizwa na maisha la hasha, upweke humpelekea mtu ajihisi vibaya mno. Kama asipokuwa na rafiki mzuri wa kumfanya arudi kwenye hali yake ya awali, huyu mtu kama hayupo vizuri kiroho(na Mungu wake) lazima atafanya vitu vibaya vya kumkosea Mungu.
Naamini wewe unayesoma huu ujumbe kwa namna moja ama nyingine umewahi kupitia hali hii, kama bado hongera, ila nikupe kazi hii ili kulielewa hili somo vizuri. Angalia yule rafiki yako ambaye ana kiu ya kuolewa/kuoa alafu akawa hampati yule anayemhitaji... asilimia kubwa utakuta wana hasira za karibu sana, yaani anaweza akakasirika mpaka ukashangaa hivi huyu hili jambo ndio linamfanya awe na hasira kiasi hichi!!. jua ni Upweke.
Ili kuepuka hili tatizo, kuwa na rafiki ambaye moyo wako unamkubali, na ambaye yupo radhi kukushirikisha changamoto zake, na wewe uwe huru kumshirikisha zako, na awe rafiki ambaye mnaweza kuomba Mungu pamoja.
~Samson Ernest.
+255759808081.
0 maoni:
Post a Comment