Ukikosa cha kumshukuru Mungu katika maisha yako, jiulize kwanini anaendelea kukupa pumzi mpaka leo. Kisha piga hesabu umelipa nini au una haki sana ya kuishi kuliko mwingine aliyetangulia?.
Mshukuru Mungu kwa uweza wake, kukuwedhesha kuwa imara mpaka leo, leo yako ni bora sana, jana isikuumize kichwa, jana isikupe majuto.
Tegemea kuwa bora zaidi ya jana, leo ni mhimu sana katika maisha yetu, usiinyime haki kwa maumivu ya jana, usiipe hofu kwa kuifanya iwaze sana kesho wakati leo hujaimaliza. Maliza leo vizuri kwa kufanya vitu vinavyompendeza Mungu na kuitendea haki za msingi kwa matendo yako.
Mungu amekuwa mwema kwangu, nawe naamini amekuwa mwema kwako, kwa pamoja tumrudishie sifa na utukufu.
Leo unaweza kutengeneza alama √ ama alama x ni uamzi wako.
Nakutakia matendo mema katika siku ya leo.
Samson Ernest.
0759808081.
0 maoni:
Post a Comment