LAWAMA KWA DADA WA KAZI ZA NYUMBANI.

Katika biblia wanajulikana kama vijakazi/kijakazi anayesaidia kazi za nyumbani, kwa hiyo ni watu wanaotambulika na kazi ambayo biblia inaitumbua kabisa.

Zipo shutuma nyingi zinazowagusa moja kwa moja hawa dada/mama zetu wanaofanya kazi maeneo haya ya nyumbani.

Kweli kabisa hizi shutuma za kuwatesa watoto na kuwapiga, kuweka chakula kinyesi na wakati mwingine kuweka mikojo yao kwenye chai zipo.

Kutokana na teckonojia ya internet na ulimwengu wa smartphones, haya mambo yanaonekana kwa wazi sana.

Wakati tunaendelea kusema mambo mengi kuhusu hawa ndugu zetu, nataka nikushirikishe mambo machache yanayowasibu eneo hili;

MSHAHARA/POSHO.
Tatizo la kuwacheleweshea hawa wadada miashara yao ni sababu kubwa inayosababisha wawe na hasira ndani mwao. Huwa inashindikana wewe mwenyewe usipolipwa mshahara wako kazini, hata ile hamu ya kufanya kazi huwa inachosha sana.
Sasa huyu dada anayelipwa pesa ndogo, hajapewa ana miezi 3 unafikiri atamfanya nini mwanao anayemsumbua huku na kule.

MATUSI.
Hasira nyingi za waajiri zinaishia kwa dada hawa, hasira za mama kukwazwa na mume wake zitaishia kwa dada, hasira za ofisini kwake zitaishia kwa dada, hasira za madeni ya vikoba yatashia kwa dada wa kazi.

KUCHELEWA KUPUMZIKA.
Huyu dada aliyelala saa tano/sita usiku ndiye anayepaswa kuamka saa kumi alfajiri, andae chai, afanye usafi wa nguo za mtoto aliyejichafua usiku.

KULA CHAKULA KIVYAKE.
Wengi wa waajiri huwa hawapendi kula meza moja na dada zetu, wanaonekana hawana hadhi. Na wakikaa meza moja maneno mengi ya kuumiza moyo wake yanakuwa yametawala mazungumzo.

KUTAKWA KIMAPENZI.
Baba mwenye nyumba anamsumbua huyu dada, kama ana watoto wa kiume nao wanamtaka kimapenzi. Hii ni familia isiyo jiheshimu na isiyo na hofu ya Mungu.

KUSHINDWA KUFANYA BAADHI YA KAZI.
Sio kila kazi huyu dada ataziweza, Labda ametoka nyumba ambayo huenda haijawahi kuwa na sakafu/terelizi/marumaru. Leo hii anaambiwa azifanyie usafi, kwa haraka haraka hili zoezi litakuwa gumu kwake.
Mwingine ametoka familia ambayo inafua nguo mara moja kwa wiki yaani pea mbili zinavaliwa wiki. Leo anakutana na rundo la nguo.

Baada ya hayo mambo machache niliyokushirikisha hapo juu, naomba uchukue tukio la kutolipwa pesa zake na unganisha na tukio la kuchelewa kulala, unganisha na tukio la kutukanwa/kufokewa kila saa.

Tafakari haya machungu yote huwa anaenda kuyatolea wapi, ikiwa dada mwenyewe hata kwenda ibadani huwa hutaki aende kwa kisingizio cha kazi nyingi.

Mtu yeyote asipokuwa na neno la Mungu ndani ya moyo wake, na akakosa mafundisho ya neno la Mungu. Huyo mtu ni hatari sana pale unapomkosea, moyo wake unakuwa umejaza kisasi. Anapokaa yeye anawaza kulipiza kisasi.

Uhitaji wa dada/ mama zetu wa kutusaidia kazi upo tena hatuwezi kuukwepa kabisa, maana hili limeonekana hata kwenye biblia walifanyika msaada mkubwa.

Hebu tuonyeshe upendo kwao na kuwalipa sitahiki zao kwa wakati. Ili kuepuka kuwashawishi watufanyie mambo ya ovyo kwa watoto wetu.

Utaniambia wapo sio waaminifu hata umtendee jema atakutendea baya, upo sawa kabisa wapo...kwani wala rushwa huwa hawalipwi mishahara yao? Hiyo ni roho ya mtu, unachopaswa wewe ni kumfahamu vizuri unayetaka akusaidie kazi.

Kabla dada wa kazi hajawa hatari kwako, epuka wewe kuwekeza sumu ndani ya moyo wake.

Ndg. Samson Ernest.
+255759808081.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

  1. Replies
    1. Asante Obadia Luyagaza. Endelea kutembelea mtazamo wa maisha.

      Delete