NITAFANYA TU NIKIFIKISHA UMRI FULANI.

Siku nyingine tena tumeiona ni jambo la kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu.
Vijana wengi wameshindwa kufanya mambo ya kufikia mafanikio na kupoteza muda na kujifariji kuwa wakifika umri fulani ndio watafanya.

Umeajiriwa ni muda wako wa kutimiza yale machache uliyopanga maishani mwako yaani fanya kazi kama unastafu kesho nakwambia wafanyakazi wenzio mwanzo watakuona ni mwoga wa maisha ila mwisho watakuheshimu na kukupongeza maana wao watakuwa wamebanwa na majukumu ya kifamilia huku anatakiwa atengeneze kitu kingine kabla hajastafu lakini inashindikana.
Ndio maana wengi wanastafu leo kesho unasikia amenunua gari ama ameanza kujenga nyumba hajui kuwa hiyo ni pesa ya kumsaidia matumizi ya kawaida, nyumba anashindwa kuimaliza huku gari nimepata tatizo linatakiwa kutengenezwa inakuwa ni miingiliano ya mambo hapo ndipo wengi presure hupatikana baada ya miezi kadhaa unasikia amefariki. Usiruhusu haya yote yatokee anza kutengeneza maisha yako ukiwa bado kijana.
Tumia nguvu ulizonazo sasa kufikia mlima wa mafanikio usifuate kauli za kula ujana wakati hujui uzee utaulisha nini.
Ishi kama kesho hutakuwa hivyo ulivyo leo.
Nakutakia kazi njema na utafutaji mwema.
SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment