Ni siku nyingine tena kumekucha na pilika za kila siku.
Leo nataka kuongelea kwa nini hujiamini kama unaweza, tumekuwa na fumo wa kuona ya kwamba kuna baadhi walizaliwa na bahati zao za kufanikiwa na kuona wengine wamezaliwa maskini tu hata wafanyaje hawawezi kufanikiwa.
Huo ni mtazamo mmbaya sana na haufai, kila mwanadamu alikuja duniani kwa kusudi maalumu na ana nafasi hapa chini ya jua kufanya kukamshangaza mwingine na mwingine.
Ishi kwa kujua ya kuwa wewe ni wa tofauti na una uwezo wa kufanya jambo kubwa maishani.
Kuzaliwa kwenye familia maskini sio kana kwamba wewe ni maskini, unapaswa kuchukua hatua ya kuelekea kwenye mafanikio.
0 maoni:
Post a Comment