Unatumia njia gani kujihamasisha pale unapokwama kufikia malengo yako.

Nikusalimu ndugu msomaji wa Mtazamo Wa Maisha na makala zake, habari za leo, matumaini yangu unaendelea vyema kung'ang'ana kwa kila linalowezekana kuhakikisha mwaka huu haupiti bila kutimiza yale uliyoahidi mbele za watu kuyafanya, na yale uliyojiahidi wewe mwenyewe kujitimizia/kujifanyia katika maisha yako binafsi. Haya yote hayaji kwa bahati mbaya ndio maana ule mwendo na kasi uliyokuwa nayo wakati unaandika malengo yako ya mwaka haifanani na matokeo ya kile ulichokianzisha au ulichotegemea kukianzisha, hizi hali zote kuna uwezekano mkubwa sana ukawa unapitia sasa pasipo kujua ufanyaje ili upate kuwa na ile hamu ya mwanzo kuendelea kukazana pasipo kukata tamaa.

Mara nyingi tumekosa hamasa ndani mwetu kwa yale malengo yetu tuliyopanga katika maisha yetu, hizi hali huwatokea wengi wetu, unaweza ukawa mmoja wapo kati ya watu walioahidi wafanye vitu fulani mwaka huu lakini umejikuta umesahau kwa kutokuandika, ama umeacha baada ya kukutana na vikwazo viwili vitatu mbele yako, labda mwaka huu ulipanga kufunga ndoa na mchumba wako ikatokea akavunja uaminifu kwako mkaachana kwa maumivu makali sana, na sasa hutaki kabisa kusikia hizo habari za kuoa/kuolewa, unamwona kila mwanamke/mwanaume hafai kwako! Ulipanga mwaka huu uwe mwaka wako wa kujiwekea Akiba kwa kila kiasi cha pesa utakachokuwa unakipata lakini mpaka leo ni September 07/2015 huoni matokeo yeyote mazuri zaidi ulichoanza kukiweka umekitumia kwa matatizo yaliyojitokeza ghafla mbele yako kwa kuugua/kuuguliwa sana na mzazi/mtoto/mke/mume/ndugu ama jambo lolote lile lilopelekea utoe kile kiasi ulichokuwa nacho kwenye Akiba, ulipanga mwaka huu utaongeza wateja kadhaa kwenye bidhaa zako unazouza ila mpaka sasa umeachana na huo utaratibu baada ya kuona hakuna mwitikio mzuri wa watu baada kutumia kila mbinu za kutangaza biashara yako, wafanyakazi wako wamekosa hamasa na mwamko kwa kile mlichoahidiana, umejaribu mpaka kuanza kuwafukuza wengine kazi kwa uzembe wao wa kutotimiza majukumu yao kwa usahihi lakini pamoja na hayo yote bado huoni matokeo yeyote mazuri ya kuleta mabadiliko bora zaidi na viwango zaidi kwa vile ulivyotarajia kuvipata.

Mwingine alipanga mwaka huu ulikuwa mwaka wake wa kusoma kozi fulani ili kujiongezea maarifa lakini imefika muda ameamua kuachana hiyo habari, mwingine alipanga mwaka huu utakuwa mwaka wa kujifunza kupitia usomaji wa vitabu mbalimbali kwa waliofanikiwa kwa yale maeneo ninayopenda kuwa, mwingine alianzisha kurasa/blog za kuhamasisha/kusaidia watu lakini ameachia njiani baada ya kuona mwitikio mdogo wa watu, niseme kwamba kila mmoja yupo kwenye changamoto yake ila tunatofautiana namna za kuzikabili na kuzimaliza pasipo kuathiri chochote, kwa ujumla kila mmoja anajua amepatwa na nini iliyomfanya aache badala ya kufanya, je unapokutana za hizi hali unafanyaje?

Unapoandika malengo yako ya mwaka lazima kuna kitu kimekufanya utamani kufanya/kukufikia hicho kitu sio kitu ambacho kimetokea kwa bahati mbaya wala si kitu ambacho hakitoki ndani mwako la hasha! ni lazima kuna kitu kimekusuma na kukufanya ufikiri kufanya hayo na kawaida ya mtu mwenye tabia ya kujipima amefanya nini na hajafanya kipi kwa yale yaliyojiwekea ni lazima awe ameweka kumkukumbu za kuendelea kujikumbusha, siku fulani niliahidi kufanya hiki na kile mbona bado sijafanya? kufanya hivyo kuna kufanya unapata kuhukumiwa ndani mwako sasa ile kuhukumiwa ina kupa nguvu ndani mwako kuongeza juhudi hata kama ilitokea umeridhika ama umechoka baada ya kukutana na vikwazo vya kukuumiza na kukurudisha nyuma.

Kingine kwa kuwa uliweka wazi baadhi ya marafiki zako unaowaamini kuhusu malengo yako pale inapotokea wamekuuliza vipi bwana ule mpango wako wa kufanya kile kitu/jambo umefikia wapi mbona kimyaa sana? hiyo itakufanya uhamasike zaidi ndani mwako na itakufanya ujisikie vibaya kwa kuongea uongo kwa watu mnaoheshimiana nao, hii itakusuma kwa nguvu kutimiza kile ulisema mbele yao japo ni chako na kina manufaa kwenye maisha yako si wao ila ile kutaka usionekane Mwongo na mtu mwongeaji tu asiye na kutimiza zile ahadi zake, kwa hali hiyo utajikuta tayari umefanya pasipo kukata tamaa na kawaida ya wanamafanikio hupenda kutoa mrejesho kwa kile alichokiahidi, huwezi kwenda kutoa mrejesho wa kushindwa pasipo kutoa suluhisho baada ya kuona mbinu ya kwanza imekwama ukachukua/ukapata wazo lingine ukalifanyia kazi na likakuletea matokeo/mafanikio makubwa/mazuri kwa kile ulichokiahidi mbele za watu.

Ili usikate tamaa na kuacha kile ulichokipanga, tumia njia moja wapo kati ya hizo hapo juu uliyoona inafaa kukuhamasisha kufikia malengo yako pasipo kuvunjika moyo, elewa wanakomaa mpaka dakika ya mwisho ndio wale wanaofanikiwa, hakuna miujiza itakayokukuta ukiwa umekaa pasipo kujaribu na kufanya kwa bidii, utaona muujiza pale utakapofikia ukomo wa akili zako na kujiuliza sasa hapa nitafanyaje? mbona naona giza? hapo ndipo Mungu huleta wazo lake moja tu ndani mwako tena unasema ngoja nijaribu haka ka njia wakati napumzisha akili ya kupata wazo zuri la kufikia malengo yangu... hapohapo unafanya hicho kidogo unajikuta upo ndani ya kile ulichokitesekea mwezi/miezi au miaka na miaka.

Usije ukaacha wala usije ukakata tamaa kwa maumivu yeyote yale utakayokutana nayo kwenye kujaribu kutimiza ndoto zako, hakikisha mlango wa kwanza wa kutokea umeshindikana kutoka, na hakikisha umeondoka na mafunzo ya kutosha kufanya vitu vya tofauti kukutoa hapo ulipo, elewa hutohamasika kwa vitendo na kuendelea kuogopa kuthubutu kile ulichopanga kufanya hutofikia malengo yako kamwe, jihamasishe huku unaendelea kufanya kidogo kidogo hata kama huoni matokeo mazuri na ya haraka kwa unachofanya, huko huko mbele kwa mbele katika safari yako utapata wazo zuri zaidi na utagundua kitu ambacho hukukitegemea kukipata maishani mwako.

Nikutakie mafanikio mema kwa kile ulichokianzisha, usiache kujikumbusha ulijiahidi/uliahidi nini.
Endelea kutembelea mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA na usiache kuwashirikisha  wengine uliyojifunza humu, waweza share zaidi kwenye mitandao ya kijamii maana huwezi jua utamsaidia nani katika kufanya hivyo.

Kwa msaada zaidi wa mawasiliano ya haraka na karibu, piga simu au tuma sms kwa whatsApp 0759808081, email; samsonaron0@gmail.com, karibu sana.
Rafiki yako Samson Ernest.

TUTAHAKIKISHA TUNAFIKA.

SHARE

Samson Ernest

Habari, mimi ni mwandishi na mhamasishaji ambaye ninapenda kuona maisha ya kila mtu yakiwa bora. Naamini kila mmoja wetu anaweza kuwa na maisha mazuri kama ataamua hivyo. Karibu ujifunze kupitia mtandao huu wa MTAZAMO WA MAISHA.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment