Karibu sana tubadili mitizamo yetu hasi kwenye fahamu zetu kwa kuingiza mitizamo chanya kwa kujifunza namna ya kukuza maeneo yako ya mauzo katika bidhaa zako, nikusalimu rafiki, habari za leo rafiki na mfuatiliaji mzuri wa makala za MTAZAMO WA MAISHA, matumaini yangu bado hujachoka kuboresha maisha yako, naamini unapambana kila siku kuikataa sauti ya kushindwa na umekazana kuiboresha sauti ya ushindi kwa kujiimarisha maeneo mbalimbali ya biashara yako kama hivi unavyosoma ukurasa huu, ni hatua moja ya wewe kuonyesha upo makini na unahitaji kukua zaidi ya hapo ulipofikia. Wakati tumebakiza siku ya leo na kesho tuumalize kabisa huu mwezi wa tisa, nina imani ulijiwekea malengo mengi na makubwa sana mwaka huu katika kukua kwenye biashara yako, ulijenga twasira kubwa ya kufika mbali kibiashara, ulijenga picha kubwa ya kukua zaidi kimtaji, ulijenga picha kubwa ya kuongeza wateja wengi zaidi ya mwaka jana, umejitahidi kubanana na wafanyakazi wako ili ufikie malengo lakini unaona kama vile upo palepale, umejaribu kujenga vitisho vingi kwa wafanyakazi wako ila unaona wanazidi kukuogopa wewe ila ukuaji wa mauzo ya bidhaa zako upo palepale wakati mwingine unazidi kudidimia zaidi chini, mpaka umefikia wakati umeanza kukimbiwa na wafanyakazi, baada ya siku mbili tatu unamwona kwa mpinzani wako.
Unaweza ukatafuta sababu yeyote ile ya kujifariji na kuwajengea picha waliobaki kuwa mwenzao amepotea kwa uamzi aliochukua, wewe ulikuwa una mlipa mshahara/posho nzuri, hayo yote unaweza kuwafunga fahamu wale waoga ambao miaka yote upo nao na wamekuvumilia kwa madhaifu yako, ila huwezi kuubadili ukweli kwamba wewe huwajali wale wanakusababisha ukue zaidi kimauzo.
Ufanye nini sasa baada ya kukutupia hizo lawama zote wewe?
Unachotakiwa kufanya, cha kwanza kabisa ni kukaa na timu yako kuieleza malengo yako katika kuikuza biashara yako, wape mrejesho kwa kile walichokifanya hapo nyuma, wape pongezi kwa bidii walioifanya kuifikisha biashara yako hapo ilipo, ikiwezekana wape zawadi wale waliofanya vizuri zaidi ya wenzao, hili la zawadi ni mhimu sana, litaonyesha ni kiasi gani unatambua mchango wao wa kufanya vizuri yale majukumu uliyowapa wafanye.
Kingine jua zaidi maisha ya mmoja moja yaani fahamu anapoishi mfanyakazi, jenga nao mazingira ya kukueleza changamoto wanazokutana nazo kwa wateja, kaa nao karibu zaidi wakueleze wanayokutana nayo kwenye familia zao, hii itakusaidia kujua namna ya kuzungumza na kila mmoja pale anapoonyesha kukwamisha biashara yako isikue. Kuwa mkali kila siku kwa wafanyakazi wako haiwezi kuleta maana ya wewe kuheshimiwa wala haiwezi kuleta maana ya wewe kuogeza ukuaji wa mauzo, kuzuia sana wafanyakazi wasikupe matatizo yao ya kifamilia haiwezi kubadili ukweli wa mambo, kwanini nasema hivi; sisi ni binadamu na ukimweka huru sana mtu anaweza kukuzoea vibaya na kukuzoea hivyo anaweza akaanza kupuuza baadhi ya majukumu yake uliyompa kwa sababu anajipa moyo mimi na boss wangu watuna shida, kwangu hana namna lazima akubali ninachomwambia hata kama kiwe cha uongo, hii ipo na unaweza ukawa mkali kila siku kuepusha hili ila bado utakuwa hujajua kutofautisha nyakati za kuzungumza na timu yako, lazima wakujue kabisa huna masihara kwenye kazi, inapofika wakati wa kila mmoja kuwajibika huna utani kabisa na inapofika wakati wa kucheka na kutaniana hauna tatizo pia eneo hilo.
Ukifika kiwango cha kujiheshimu na kuwaheshimu wao, utajikuta hutumii nguvu kubwa ya kuwasukuma wafanye kile unataka wafanye, pia unatakiwa uwe mwangalifu wa kutoonyesha sana upendeleo wa kumsikiliza tu yule anayekuletea faida kubwa kwenye bidhaa zako, kwanini uwe mwangalifu kwa huyu mtu? upo uwezekano mkubwa wa kuharibu timu yako ya mauzo kwa ajili ya mfanyakazi moja kwa sababu wengi wao hujaa kiburi cha hakuna anayeweza kunifikia mimi, bila mimi hii ofisi isingekua hivi, bila mimi huyu boss asingefika hapa, bila mimi hawa wenzangu hawezi kitu... huyu mfanyakazi anaweza akawa sahihi kabisa na ukweli ndani yake ila anapoonyesha majivuno ya dharau kwa wenzake na kuwaambia maneno ya kejeli inawavunja moyo wale wachanga kifikra na wale wageni ambao hawana muda mrefu kwenye ofisi yako, unachotakiwa kufanya/kujua ni kwamba anayefanya vizuri wenzake wamjue kwa mtazamo wa kujifunza kwake na si umfanye awaone wenzake hawana kitu, kumbuka kila kiungo kwenye biashara yako kina umhimu, mkono wako wa kulia unaweza ukawa na nguvu kubwa kuliko wa kushoto ila hapohapo kuna kazi zingine huwezi kufanya kwa kutegemea mkono mmoja. Tathimini viungo vyote katika biashara yako, kila mmoja mpe nafasi yake kutokana na uwezo binafsi alionao, kufanya hivi utawainua hata wale wadhaifu, hakikisha huondoi mfanyakazi bila kujua ameshindikana kuelimika na kubadilika kwa yale unayomwelekeza ndio umwondoe haraka sana kuepusha kuendelea kukuingiza hasara zaidi.
Urafiki na ukaribu wako wa timu yako unajenga utofauti mkubwa wa ukuuaji wa bidhaa zako maana watafanya kazi kwa moyo na kwa bidiii kubwa mno, watakuwa na usikivu/umakini pale unapowaletea changamoto unayopitia muda huo kwenye biashara yako. Kingine cha mwisho kabisa usiogope kuwaeleza mzigo uliopo sasa kwenye stoo na wambie kabisa wasipofanya bidii kuumaliza kwa kuusambaza haraka sokoni mpinzani wako atakuwahi na mtaingia hasara kubwa, inaeleweka kwamba kushuka kwa mauzo ni kushuka kwa mshahara/posho/kamisheni kwa mfanyakazi.
Nikutakie ufanyiaji kazi kwa yale unayoona yanafaa kufanyia kazi kwenye eneo lako la biashara, na kama unafanya kila kitu kwenye biashara yako na hutaki wafanyakazi nakuomba ukafikiri kwa upya, hakuna tajiri dunini aliyefika hapo alipo kwa kufanya kazi zote peke yake, tuna masaa 24 tu kwa siku, kwa kifupi hayatutoshi bila kusaidiana majukumu.
Mimi rafiki yako Samson Ernest, email; samsonaron0@gmail.com/mtazamowamaisha@gmail.com
Wasap; 0759808081.
Asante sana kwa kunipa muda wako.
0 maoni:
Post a Comment